Kamati ya Maadili ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi CCM, imewahoji wabunge Jerry Silaa (Ukonga) na Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Humphrey Polepole kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dodoma.

Wabunge Jerry Silaa na Josephat Gwajima wametakiwa na kamati hiyo kufuatia wito uliotolewa na Spika wa Bunge, Job Ndugai baada kukutwa na makosa mbalimbali na kamati ya Haki Maadili na Madaraka ya Bunge.

Katibu wa Wabunge wa CCM, Rashid Shangazi amesema Chama Cha Mapinduzi kwenye muhimili wa Bunge wamewaita wanachama hawa ili kuwahoji kuhusu masuala tofauti.

Kufuaia agizo hilo leo asubuhi Mbunge Silaa na Polepole kwa nyakati tofauti wamefika kuhojiwa na Kamati hiyo ya Maadili ya Wabunge wa CCM.

Baada ya kikao hicho Polepole akizungumza na waandishi wa habari amesema kikao cha Maadili ni kikao cha ndani hivyo taarifa zote zitatoka kwa utaratibu wa Chama.

EU kuunda kikosi maalumu kwaajili ya kukabiliana na Taliban
Mayele awatuliza mashabiki Young Africans