Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey PolePole amesema kuwa chama hicho kimeanza kufanya mageuzi ya makusudi ili kukirejesha kwenye misingi ya kuanzishwa kwake.

PolePole amesema kuwa mageuzi hayo ya makusudi yana lengo la kukifanya chama kuwa cha watu, kuwasikiliza na kusimamia maslahi ya wanyonge ili kurejesha imani kwao katika vitendo vyote vinavyo fanywa na chama.

“Kila mtu anahitaji kuthaminiwa na kuhifadhiwa utu wake bila kujali hali yake,CCM haichukii watu wenye mali wala masikini, bali inakerwa sana na watu wanaopata utajiri  wao kwa njia za hila kama kukwepa kodi, dhuluma na kupora watu” amesema PolePole.

Aidha amesema CCM kama chama cha wananchi, kitajinasibu kwa umma kwa kuondoa shida zao na kuongeza kuwa kuhusu mchakato wa Katiba na changamoto zilizopo katika muungano wananchi wa pande zote chama kitawasikiliza.

Hata hivyo PolePole ameongeza kuwa mzunguko wa fedha kwa sasa ni mgumu kwa kuwa Rais anapambana na wale ambao walikuwa wakizipata kwa njia zisizo halali.

Polepole atangaza moto wa 'mageuzi ya makusudi' CCM
Mbowe avunja Ukimya kupotea kwa Saanane, atahadharisha ‘maneno’