Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole amesema kuwa Mbunge wa Kigoma mjini kupitia tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe mwaka 2020 atafute kazi nyingine ya kufanya kwa sababu jimbo hilo litarudi kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Polepole amesema hayo wakati akifanya ukaguzi wa mradi wa kusambaza maji mkoa wa Kigoma ambapo amesema kuwa wanataka kuhakikisha kuwa mkoa huo unapata maji safi kabla ya mwaka 2020.

“Mkandarasi ameniahidi mpaka mwezi wa tano maji yataanza kutolewa kwa karibia asilimia mia moja katika mji wote wa Kigoma Ujiji na maeneo ya pembezoni na mimi nimezungumza na viongozi wenzangu wa CCM wafike hapa mwezi mmoja kutoka leo kujiridhisha juu ya maendeleo ya kukamilisha mradi huu na kupeleka maji katika mji wetu wa Kigoma , sisi tunafanya hivi sababu tunao mkataba na wananchi na tunataka kuukamilishe mapema kabisa kabla ya 2020 ili ifikapo 2020 basi mbunge wa hapa atafaute kazi nyingine,”amesema Polepole

Hata hivyo,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole yupo mkoani Kigoma katika ziara ya Kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mwaka 2015 – 2020.

 

 

Makonda kutengeneza ajira vikundi vya kukimbia
Jafo aagiza wakuu wa mikoa kukabiliana na ombaomba