Afisa wa Jeshi la Polisi Mtwara Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Grayson Mahembe, ambaye ni miongoni mwa maafisa saba wa jeshi hilo waliofunguliwa mashtaka ya mauaji ya mfanyabiashara, amejinyonga

Askari huyo alijinyonga Januari 22 mwaka huu kwa kutumia tambala la kudekia akiwa mahabusu ya kituo cha polisi wilaya ya Mtwara.

Mwili wa Grayson ulizikwa kijijini kwao Iladutwa wilayani Iringa, huku mamia ya waombolezaji wakishiriki msiba huo.

Katika taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mtwara ACP Mark Njera, alikiri kuwa askari wake saba wanaotuhumiwa kutekeleza mauaji ya kijana Mussa Hamisi (25), mkazi wa kijiji cha Ruponda wilaya ya Nachingwea mkoani humo aliyekuwa akiwadai askari hao zaidi ya shilingi milioni 33.7 wameshafikishwa mahakamani

Imeelezwa kuwa tukio la mauaji ya kijana huyo walilitekeleza Januari 5, 2022 na mwili wa marehemu waliutupa katika kitongoji cha Majengo, kijiji cha Hiari wilayani Mtwara.

Biden kumuwekea vikwazo Putin
Makamu wa Rais awapa maagizo mabalozi