Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu limechukua hatua ya kumfukuza kazi askari wake anaedaiwa kumtorosha mtuhumiwa wa Mauaji.

Kamadanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Onesmo Lyanga amewaambia waandishi wa habari kuwa Jeshi hilo limechukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa askari huyo kwa makusudi alimtorosha mtuhumiwa huyo wa mauaji katika kituo cha Luguru wilaya ya Itilima mkoani humo.

“Februali 2, mwaka huu katika Kituo cha Polisi Lugulu, askari alimtorosha mtuhumiwa wa kesi ya mauaji Itl/Ir/95/2016, mkazi wa Kijiji cha Gambasingu wilayani Itilima,” alisema Kamanda Lyanga.

Alisema kuwa askari huyo amelidhalilisha Jeshi la Polisi na kwamba atafikishwa mahakamani haraka kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Aidha, Kamanda Lyanga alieleza kuwa Jeshi hilo linawashikilia askari wengine saba kwa uchunguzi wakituhumiwa kuwatorosha watuhumiwa watatu wa mauaji na ujangili katika mkoa huo.

Alisema kuwa Januari 19 mwaka huu, askari hao walisababisha watuhumiwa hao kutoboa ukuta na kutokomea pasipojulikana.

Picha: Huyu ndiye msanii wa kike anayemiliki 'gari' wa gharama zaidi Tanzania
Marekani yamtumbua Jipu Mtanzania gwiji wa dawa za kulevya duniani