Nchini Marekani afisa wa polisi Garrett Rolfe, aliyemuua Mmarekani mweusi katika mji wa Atlanta anaweza kushtakiwa katikati ya wiki hii, kulingana na mwendesha mashitaka mkuu wa kaunti ya Fulton, Paul Howard.

Howard amesema ofisi yake itazungumza na mashahidi wengine wawili, kabla ya kufanya uamuzi wa kufungua mashtaka dhidi ya afisa, Garrett Rolfe.

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Marekani, CNN, Howard amekieleza kituo hicho kwamba Brooks hakuonekana kama ni tishio kwa mtu yeyote, kwa hiyo hakukua na haja ya kumuua.

Kulingana na uchunguzi wa jimbo la Georgia, afisa huyo wa polisi alimpiga risasi Rayshard Brooks mwenye umri wa miaka 27 akiwa nje ya mgahawa mjini Atlanta Ijumaa usiku, baada ya kijana huyo kukataa kukamatwa.

Brooks alifariki kwa kupozeta damu nyingi, baada ya kupigwa risasi mbili mgongoni.

Majaliwa: vijana msifuate mabinti, miaka 30 itawasubiri
Carragher apasua ukweli usajili wa Timo Werner