Kamanda wa Idara ya Polisi ya New York nchini Marekani, Emanuel Gonzalez anachunguzwa kwa tuhuma za kuwataka askari wake kumpiga risasi rapa 50 Cent pindi watakapomuona.

Kwa mujibu wa New York Daily News, 50 Cent na kamanda huyo walikuwa na mtafaruku wa siku nyingi.

Gonzales anadaiwa kutamka hayo Juni 7, 2018 alipokuwa katika eneo la kuhesabu namba, muda mfupi kabla ya 50 Cent kutaka kuingia katika eneo hilo kuangalia mchezo wa masumbwi ulioandaliwa na jeshi la Polisi.

“Inspekta alisema hayo wakiwa kwenye eneo la kuhesabia namba,” chanzo kimoja kiliiambia Daily News.

Gonzalez anadaiwa kujaribu kuipundua kauli hiyo na kuifanya kuwa utani, lakini taarifa hiyo iliyochukuliwa kwa umuhimu imesambaa kwa kasi.

Jana, rapa huyo alionesha kukasirishwa na kitendo kilichofanywa na Gonzales na aliahidi kumchukulia hatua za kisheria.

“Hivi ndivyo nilivyoamka leo asubuhi. Huyu mtu Emanuel Gonzales ni askari mchafu anayetumia madaraka yake vibaya. Kinachosikitisha ni kwamba huyu mtu bado yuko ofisini na ana beji na bunduki. ninayachukulia kwa umakini mkubwa haya na nawasiliana na mwanasheria wangu ili tuone kinachofuata,” 50 aliandika kwenye Instagram na Twitter.

Mwezi mmoja uliopita, Gonzales aliwahi kufungua mashtaka ya unyanyasaji dhidi ya 50 Cent.

Fatma Karume aeleza sababu za kuachana na Urais TLS
Bilioni 27.4 zapitishwa bajeti ya 2019-2020 Njombe

Comments

comments