Polisi wa Los Angeles, Greg Kading ambaye amekuwa akisimamia kesi ya mauaji ya marapa nguli na mahasimu, 2 Pac Shakur na Notorious B.I.G amedai kuwa Sean Combs aka Diddy alihusika kupanga mauaji ya 2 Pac.

Kading ambaye alikuwa mmoja kati ya askari waliteuliwa mwaka 2006 kuunda kikosi kasi cha kufuatilia kesi za mauaji ya kupigwa risasi ya marapa hao, aliiambia Huffington Pos kuwa Diddy alilikodi kundi hatari la kihalifu la ‘Crips’ kiasi cha $1 million kumuua 2 Pac.

Alieleza kuwa usiku wa Septemba 7 mwaka 1996, memba wa kundi la Crip, Duane Keith maarufu kama Keffe D alitekeleza maagizo ya Diddy na kumpiga risasi Shakur ambaye alikuwa na meneja wake, Marion Hugh aka Suge Knight.

Hata hivyo, alieleza kuwa aliyefyatua risasi zilizompata 2 Packati ya waliokuwa kwenye gari la wauaji hao ni mpwa wa Keffe D anayefahamika kwa jina la Orlando ‘Baby Lane’ Anderson.

Kading alieleza kuwa alijaribu kuwaeleza Polisi wa Los Angeles kumfungulia mashitaka Diddy, lakini walikataa. Anasema anadhani chanzo cha kupotezea kumkamfungulia mashtaka Diddy ni umaarufu wa mwanamuziki huyo aliyekuwa meneja wa Notorious B.I.G.

Lakini pia ameeleza kuwa huenda ni kwa sababu mfyatua risasi, Orlando ‘Baby Lane’ Anderson alishafariki.

Hata hivyo, Diddy amekanusha vikali taarifa  za Kading na kuzitaja kuwa uongo na uzuzushi wa kipuuzi.

Baada ya kuona hasimu wake amepata tuhuma hizo, 50 Cnet naye alizichochea kwenye Instagram.

 

Wachina waadhimisha mwaka mpya wa Nyani kwa mtindo wa pekee
Mwanasheria azungumzia uzushi wa kifo cha Gwajima