Diwani wa Kata ya Mabatini, Deo Mbibo pamoja na watu takribani 20 wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanashikiliwa na polisi baada ya kukamatwa walipokuwa wameenda kuhani msiba wa mwanachama mwenzao.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza, Leonard Nundi, ambapo amesema kuwa tukio hilo limetokea ambapo wafuasi hao wakiwa zaidi ya 500 walienda kuhani msiba huo na ghafla polisi waliwavamia na kumtaka mfiwa kuongea naye.

“Chanzo cha vurugu ni baada ya askari hao kuvamia msibani na kumhitaji mfiwa ambaye ni Laurent Chiro kwa ajili ya mazungumzo, waliposhindwa kuelewana walimchukua diwani na viongozi wengine waliokuwa meza kuu na kuwapandisha kwenye gari la polisi,” amesema Nundi

Hata hivyo, amefafanua kuwa wanachama waliokuwa msibani waliogomea kitendo hicho walianza kuwarushia mawe polisi ambao nao walijihami kwa kupiga mabomu ili kuwatawanya.

 

Mourinho awashangaa wanaoishangaa Manchester United
Auawa baada ya kufanya mapenzi na Ng'ombe