Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam imekusanya mapato ya zaidi ya sh. million mia tano kupitia kikosi chake cha usalama barabarani kuanzia tarehe mei 20 mwaka huu mpaka mei 29.

Akiongea na waandishi wa habari leo Kamishna wa jeshi la polisi kanda maalum Dar es salaam Simon N Sirro amesema fedha hizo zimetokana na makosa mbalimbali yaliyofanyika barabarani kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Akianisha aina ya tozo zilizofanywa na wanausalama barabarani Kamishna Sirro ametaja jumla ya magari yaliyokamatwa ni 14,788, pikipiki 3484, daladala 3520, na kutaja jumla ya makosa ni 18,272 na kufanya jumla ya fedha za tozo kufikia 548,160,000.

Aidha katika taarifa nyingine Jeshi la polisi kanda maalumu linawashikilia wamiliki sita wa madanguro na jumla ya madada na makaka poa 23.

Wakati akizungumza na vyombo vya habari kamishna Sirro amewataka wafanyaji wa biashara hiyo haramu ya kuuzwa na kuuza miili waache mara mioja kwani hatua kali zionaendelea kuchukuliwa dhidi yao.

Kamanda sirro  amewakamata washtakiwa hao mnamo mei 26 wakati wa oparesheni ya kukomesha biashara hizo ambazo zipo kinyume cha sheria pamoja na maadili ya nchi.

Akiwataja kwa majina wamiliki wa madunguro hayo ni Chiku Msafiri,  Zaina Mussa, Hellene Newe, Mrisho Khalifan, Ally Mwinyimvua, na Diula Victor wakazi wa wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

 

 

Wabunge wa Ukawa, CCM wamgomea Naibu Spika kukataa hoja ya wanafunzi waliofukuzwa UDOM
Maafande Wa Ruvu JKT Watoa Mchezaji Bora Wa Mwezi