Leo leo December 6, 2016 imetolewa taarifa ya uchunguzi wa madaktari kuhusu kifo cha mchezaji wa timu ya Mbao FC chini ya umri wa miaka 20, Ismail Khalfan aliyefariki dunia siku ya Jumapili ya December 4, 2016 baada ya kuanguka uwanjani Kaitaba wakati wa mchezo wao dhidi ya timu ya vijana wa Mwadui ikiwa ni mechi ya mwisho ya kumaliza mzunguko wa kwanza wa ligi ya Vijana.

 Baada ya uchunguzi wa Madaktari Jeshi la Polisi limetoa ripoti hiyo ambayo imeeleza kuwa mchezaji huyo alifariki uwanjani kutokana na kupata tatizo la kusimama ghafla kwa moyo (sudden Cardiac Arrest-SCA).
dv2a0266
Kamishina Augustin Ollomi amesema mchezaji huyo hakuwa na jeraha lolote ila Madaktari walibaini kusimama ghafla kwa moyo na kupelekea kifo chake.
Ismail Khalfan amefariki akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mjini Bukoba.
Kabla ya kufariki dunia, Ismail aliifungia timu yake bao la kwanza na bao la pili lilifungwa kwa mkwaju wa Penati hivyo mtanange kumalizika kwa 2-0.
dv2a0275

Gari la zimamoto klikiondoka uwanjani Kaitaba ikiwa imebeba mchezaji Ismail kuelekea hospitali ya Mkoa wa Kagera.

Ismail aligongana na beki wa Mwadui Fc na baadae akiwa peke yake alianguka chini lakini na kutokana na ukosefu wa huduma ya kwanza na gari la wagonjwa katika uwanja huo kulipelekea marehemu kupandishwa kwenye gari la zima moto na kupelekwa hospital ambapo mauti yalimkuta njiani.
Ismail Mrisho Khalfan(kulia) akitupia shangwe kwenye Camera yetu

Ismail Mrisho Khalfan(kulia) akitupia shangwe kwenye Camera yetu

Mats Hummels Amsihi Jose Mourinho
Mzee wa miaka 75 aweka bango mtaani kusaka mke