Jeshi la Polisi nchini Kenya limeongeza uchunguzi wa shughuli za wanamgambo wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab na jitihada zao za kujipenyeza nchini ili waweze kufanya mashambulizi.

Inspekta Jenerali wa Polisi nchini humo, Joseph Boinett amesema kuwa maafisa wa usalama wamekatiza majaribio ya mashambulizi mwezi katika maeneo ya wilaya za Mandera na Wajir kaskazini mashariki Kenya.

Inspekta Boinnet, katika taarifa iliyotolewa mjini Nairobi amesema kuwa wanafuatilia kwa karibu hali zinazoendelea nchini Somalia ambapo mikoa inayopakana na nchi ya Kenya imeshuhudia ongezeko la wanamgambo wa Al-Shabaab.

Prof. Lipumba asema yupo ngangari. "kilichofanyika Zanzibar ni sawa na kikao cha harusi"
Mbowe awageuzia kibano kampuni iliyomtimua kwenye jengo la NHC