Katika kukabiliana na mabadiliko ya Sayansi na Technolojia, Jeshi la Polisi linatarajia kuja na mkakati wa Pamoja na Chuo kikuu cha Dar es salaam wa masuala ya tafiti mbalimbali ambazo zimelenga kubaini na kukomesha vitendo vya kihaLifu.

Akiongea na waandishi wa Habari, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Dkt. Lazaro Mambosasa amesema moja ya majukumu yao ni kulinda raia na mali zao.

Amesema, kupitia kitengo cha utafiti katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam wameona ni vema wafike chuoni hapo ili kujifunza masuala ya kiutafiti huku akisema malengo ya Mkuu wa Jeshi hilo, IGP
Camillus Wambura ni kuona Jeshi la Polisi linawekeza katika tafiti.

Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha Utafiti cha Jeshi la Polisi Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, Kamishina msaidizi wa Polisi, ACP Ralph Meela amesema kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia wameona vyema waje na mtazamo mpya katika kukabiliana na uhalifu.

Dkt. Mabula aipongeza Wizara ya Habari ubunifu NAPA
Tanzania, Afrika Kusini kuadhimisha siku ya Afrika