Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi Awadhi Haji amesema kwamba Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa madereva wa pikipiki (bodaboda) wanaokiuka sheria ya uvaaji wa kofia ngumu na sheria nyingine za barabarani.

Kamanda Awadhi ameyasema hayo leo kwa njia ya simu alipokuwa akieleza namna ambavyo Jeshi la Polisi linakabiliana na ongezeko la ajali za bodaboda katika Jiji la Dar es Salaam.

“Tumekuwa na operesheni ya kukamata waendesha bodaboda wanaovunja sheria za barabarani ikiwa pamoja na ukiukwaji wa uvaaji wa kofia ngumu kwa madereva na abiria wa bodaboda na wamekuwa wakilipishwa faini au kupelekwa mahakamani,” alifafanunua Kamanda Awadhi.

Aliendelea kusema kuwa, kwa sasa mwitikio wa uvaaji wa kofia ngumu kwa madereva na abiria wa bodaboda ni mkubwa kwani wengi wao wanatii sheria hiyo na kwa wachache wanaokiuka huchukuliwa hatua kali.

Mapema mwezi Juni, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda alilitaka Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua kali madereva wa bodaboda na abiria wanaokiuka kuvaa kofia ngumu.

Mhe. Makonda amesema kukiuka kuvaa kofia ngumu kwa dereva na abiria wa bodaboda ni tukio la kujaribu kujiua. Hii imetokana na ongezeko kubwa la ajali za bodaboda nchini ambazo zinakatiza maisha ya watanzania wengi

Jose Mourinho Arusha Dongo kwa Babu Wenger
Serikali Kulinda Afya Ya Jamii