Hali ya taharuki imezuka nchini Haiti, kufuatia mauaji ya wa maafisa sita wa polisi waliouawa na majambazi wenye silaha Wilayani Liancourt, Kaunti ya Artibonite na kuchochea maandamano ya Polisi na Raia yaliyolenga makazi ya Waziri Mkuu, Ariel Henry.

Waandamanaji hao, walichoma matairi, kuziba barabara kuu kwa msaada wa magari, ma kuzorotesha shughuli za kiuchumi katika mji mkuu wa Port-au-Prince huku Wanafunzi wakishindwa kuhudhuria masomo kuliko kawaida.

Baadhi ya Waandamanaji wakiwa katika makazi ya Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry, Port-au-Prince. Picha ya Ralph Tedy Erol / Reuters.

Maafisa wa polisi, wengi wao wakiwa wamevalia kiraia, pia walielekea katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Toussaint-Louverture, wakati Waziri mkuu aliporejea nyumbani baada ya kushiriki katika mkutano wa saba wa CELAC nchini Argentina.

Hali ya sintofahamu pia ilitanda katika mikoa kadhaa ya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na Saint-Marc ambapo maafisa wa kitengo cha wasomi cha polisi ya kitaifa, Swat Team, walifanya operesheni huko Croix-Moreau, katika wilaya ya Liancourt.

Chongolo ataka tamati ya migogoro Wakulima na Wafugaji
Caicedo atuma waraka Brighton & Hove Albion