Siku mbili kabla ya kuanza kwa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara msimu wa 2016/17, Timu mbili zilizoshushwa daraja kutoka ligi daraja la kwanza hadi daraja la pili kwa kosa la upangaji matokeo katika michuano ya ligi daraja la kwanza msimu uliopita, Polisi Tabora na Geita Gold zimejishusha daraja kwa kushindwa kufanya usajiri katika mtandao wa TMS.

Afisa Habari wa Shirikisho la soka nchini (TFF) Alfred Lucas amesema kanuni za soka zinasema kama timu haijafanya usajiri hairuhusiwi kushiriki ligi na isiposhiriki ligi inashushwa daraja.

“Kanuni zinasema kama hujajisajili huna nafasi ya kushiriki ligi, usajili wetu tunasajili kwa mfumo wa mtandao TMS. Timu za Geita Gold, Polisi Tabora hawajasajili katika mfumo huo kwa msimu wa 2016/2017, uliofunguliwa Juni,15, 2016, na kufungwa tarehe 6 Agosti mwaka huu. Licha ya hivyo baada ya maombi tulifungua usajili kwa siku mbili tarehe 13 hadi 15 Agosti lakini timu hizo hazikuitumia nafasi hiyo kujisajili,” amesema.

Kuhusu wachezaji wa timu hizo, Lucas amesema timu husika zitawajibika kulipa stahiki za wachezaji wake endapo watalalamika kutotimiziwa mahitaji yao kwa kuwa wao ndio wenye wajibu wa kuishitaki timu.

Andres Iniesta: Niliikataa Ofa Ya Pep Guaradiola
Jipya Laibuka Sakata La Dimitri Seluk Na Pep Guardiola