Kikosi cha Maafande wa Polisi Tanzania FC, kimepata ajali wakati kikitoka kwenye mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Biashara United Mara FC, utakaochezwa Julai 14.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Polisi Tanzania, kupitia akaunti rasmi ya Instagram ya Polisi Tanzania imeeleza namna hii: Timu yetu imepata ajali wakati ikitoka mazoezini leo. Baadhi ya wachezaji wameumia.

Tunaomba mashabiki wetu na wapenda michezo waendelee kuwa na subira na taarifa rasmi itakujia hivi punde.

Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Hassan Juma amesema kuwa kwa sasa wanashughulikia afya za wachezaji pamoja na wale ambao wameumia na taarifa rasmi zitatolewa.

Ufafanuzi Zanzibar kupokonywa uanachama shirikishi CAF
Tanzania yaibuka kidedea udhibiti mfumuko wa bei Afrika Mashariki