Maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa ‘JKT Tanzania FC’ wameshindwa kutamba nyubani mjini Dodoma, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na maafande wenzao wa Jeshi la Polisi ‘Polisi Tanzania FC’.

Mchezo huo uliochezwa mishale ya saa nane na kukamilika majira ya saa tisa na dakika arobaini na tano, ulichezwa kwenye uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.

JKT Tanzania waliokua na matumaini ya kubakisha alama tatu nyumbani kabla ya kipyenga cha kwanza hakijapulizwa, walitangulia kupata bao la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji Daniel Lyanga kwa mkwaju wa Penati kipindi cha kwanza.

Hata hivyo Polisi Tanzania walifanikiwa kusawazisha katika kipindi cha pili kwa mkwaju wa Penati, kupitia kwa Marcelo Kaheza.

Kwa matokeo hayo JKT Tanzania wanafikisha alama 21 zinazowaweka katika nafasi ya 14, huku Polisi Tanzania wakibaki kwenye nafasi ya 10 kwa kufikisha alama 24.

Mabalozi wamlilia Maalim Seif
Mwili wa Maalim Seif wawasili Zanzibar, kuzikwa leo