Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limebainisha kuwa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kilikiuka sheria ya udhibiti wa matumizi ya mtandao wakati zoezi la majumuisho ya kura likiendelea kufanywa na Tume Ya Uchaguzi ya Taifa (NEC).

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ameeleza kuwa kwa kutumia wataalam wa jeshi hilo kitengo cha TEHAMA wamebaini kuwa kituo hicho kilifanya kazi nje ya mipaka yake kwa kukusanya matokeo ya urais nchi nzima na kufanya majumuisho.

Alisema kuwa wakati wanaendelea na zoezi la kukusanya taarifa hizo, walikuwa walifanya pia kosa kubwa la kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii kinyume cha sheria.

“Mawakala hao walionekana wakikusanya matokeo na kuyaleta huku Dar es Salaam, na baadae zile taarifa zikaonekana zinasambazwa,” alisema Kamanda Kova.

“Inawezekana kuzikusanya lisiwe tatizo kubwa sana, lakini unapokusanya na hatimaye ukaanza kuzisambaza kupitia mitandao ya kijamii hilo ndilo kosa kubwa,” aliongeza.

Jeshi la Polisi linawashikilia maafisa 38 wa kituo hicho cha LHRC kwa tuhuma hizo tangu Octoba 29 mwaka huu.

Uongozi wa kituo hicho umelalakimia hatua ya kuendelea kushikiliwa kwa wafanyakazi hao ambao ni wanasheria wakidai kuwa shughuli zote za kituo hicho zimesimama kwa muda wa siku 7 hadi jana na kwamba wameshindwa hata kutoa ripoti yao kama waangalizi wa ndani.

 

NEC Yaweka Wazi Idadi Ya Wabunge Viti Maalum CCM, Chadema Na CUF
CCM Tanga Wavurugana, Waahidi Kufanya Maandamano