Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam, wamefanikiwa kumuua jambazi maarufu aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu anayejulikana kwa jina la Kambale, usiku wa kuamkia leo, eneo la Ukonga Mazizini, na kumkuta na silaha moja aina ya Bastola.

Kamanda wa kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ametoa taarifa kuwa, jambazi huyo alikuwa ni maarufu sana kutokana na matukio yake ya utekaji wa bodaboda na kuwaua watu.

Amesema jambazi huyo alipewa jina la kambale baada ya kuzoeleka kwa tabia yake ya kuwaua madereva bodaboda, kuwatesa bila kukamatwa kwani kila akitaka kukamatwa alikuwa anateleza.

“Katika juhudi zetu za kupambana na uhalifu, tumeua jambazi maarufu sana alikuwa anaitwa kambale, ametesa sana kule Ukonga – Mazizini na Kinyerezi, amekuwa anateka watu na kuwaua bodaboda na kufanya chochote anachotaka na jina la Kambale lilikuwa na maana ya kila akitaka kukamatwa anateleza”, amesema Mambosasa.

Aidha ametoa angalizo kuwa, bado wanaendelea kuwasaka wale wote, wanaotaka kuleta taswira tofauti ili kabla hawajatimiza lengo lao wawafikie na Jiji liendelee kuwa salama.

Kwa shilingi 3000 na 5000 utashuhudia Taifa Stars Vs Equatorial Guinea
Zimbabwe: Wafanyakazi wa Serikali wapanga maandamano mapya