Polisi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy wamepata kibarua kigumu kumtafuta paka aliyetoroka mikononi mwa abiria, Ijumaa iliyopita.

Mamlaka ya uwanja huo wa Ndege imeeleza kuwa paka huyo aliruka kutoka kwa abiria aliyekuwa anaelekea nchini China na kusababisha taharuki. Polisi waliendelea na msako hadi mmiliki wa paka huyo aliposafiri kwa ndege.

Hata hivyo, polisi walishindwa kumpata paka huyo aliyetajwa kwa jina la Pepper, ingawa abiria wengi walidai kuwa wameuona mkia wake tu!

Mwakilishi wa Uongozi wa uwanja huo wa ndege ameeleza kuwa polisi wanaendelea na jitihada za kumtafuta paka huyo kadiri iwezekanavyo.

Wameahidi kuwa endapo watampata paka huyo, watamsafirisha hadi nchini China na kuhakikisha anakutana na mmiliki wake.

 

Chanzo: Dailynews

Pacquiao aahidiwa kupigwa KO
Wananchi Njombe waiomba Serikali kukamilisha ujenzi ghala la matunda

Comments

comments