Polisi nchini Sudan wameamriwa kutofanya mashambulizi dhidi ya maelfu ya waandamanaji waliopiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi mjini Khartoum tangu Ijumaa wakimtaka Rais Omar al-Bashir ajiuzulu.

Waandamanaji hao walisikika wakipiga kelele wakisema  “uhuru, uhuru, haki – jeshi moja, watu wamoja”,.

Chanzo cha maandamano hayo awali kilitokana na gharama kubwa ya maisha lakini sasa ni ya kumshinikiza rais Bashir ambaye amekuwa madarakani kwa takriban miaka 30 sasa, ajiuzulu.

Katika taarifa yake msemaji wa polisi aliandika”Tunatoa amri kwa vikosi vyote” visiingilie “maandamano ya amani au kuwashambulia wananchi”.

“Tunamuomba Mungu asaidie kuleta utulivu nchini mwetu… na kuwaunganisha Wasudan… na kufikiwa kwa makubaliano yatakayosaidia kupokezana madaraka kwa amani,” iliendelea kusema taarifa hiyo.

Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo amesema waandamanaji saba waliuawa siku ya Jumatatu na wengine 15 kujeruhiwa, huku maafisa 42 wa vikosi vya usalama nao wakijeruhiwa pia huku watu 2,500 wamekamtwa.

Aidha, Waziri wa habari nchini Sudan amethibitisha mipango ya serikali kutatua mzozo kupitia mazungumzo na kupongeza vikosi vya usalama.

Maandamano haya yanaadhimisha miaka 34 ya mapinduzi yaliouondoa utawala wa rais Jaafar Nimeiri.

 

 

Mbarawa amtengua mkurugenzi wa Maji Mtwara
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Aprili 10, 2019

Comments

comments