Polisi nchini India wanamsaka tumbili mmoja ambaye aliiba mtoto na kutoroka naye katika jimbo la Orissa, mashariki mwa nchi hiyo.

Mama wa mtoto huyo wa kiume amesema kuwa aliona tukio hilo lakini hakuweza kumuokoa mwanae hivyo kuomba msaada kwa polisi.

Aidha, Baba wa mtoto huyo aliupata mwili wa mtoto huyo wa kiume kwenye kisima nyuma ya nyumba yao, siku moja baada ya mtoto huyo kuibwa na tumbili huyo.

Polisi wamesema kuwa tukio hilo ni la kipekee sana ingawa mara kwa mara tumbili huwa wanaharibu mali katika eneo hilo.

“Tunamatumaini makubwa kwamba tutafanikiwa kumkamata tumbili huyu katika kipindi cha wiki moja,” amesema afisa mmoja wa polisi kwa jina Pradhan.

 

JPM: Watu huko duniani wanatushangaa…
Wazambia watua nchini kuikabiri Twiga Stars

Comments

comments