Jeshi la Polisi nchini limewabana watu wenye silaha nzito wanaosadikika kuwa ni majambazi wazoefu na kupambana nao katika eneo la Vikindu, Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.

Taarifa kutoka kwa mashuhuda zimeeleza kuwa mapambano hayo yameanza usiku na kuendelea hadi muda huu huku milio ya risasi ikitawala.

Zaidi ya magari 16 ya Jeshi la Polisi yameshuhudiwa yakielekea katika eneo hilo huku askari wakiwa wameshikilia bunduki kwa umakini wa hali ya juu.

Kwa mujibu wa Mwananchi, magari yote ya abiria na binafsi yanaelekea katika maeneo hayo yamezuiwa kwa muda wakati mapambano yakiendelea.

Tukio hilo linatokea ikiwa ni siku moja baada ya watu wenye silaha kuvamia na kuwaua askari wanne wa jeshi la polisi wilaya Temeke waliokuwa wakibadilishana lindo.

Kamishna wa Operesheni ya Mafunzo ya Jeshi la Polisi, Nsato Marijani alitangaza vita dhidi ya wahalifu hao.

Breaking News: Polisi wamaliza kazi Mkuranga, yawazima Majambazi
Video: Majaliwa - Serikali italinda amani kwa gharama yoyote