Jeshi la Polisi jijini Mwanza jana liliwazuia viongozi na wafuasi wa Chadema kuuchukua mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Geita, Aliphonce Mawazo katika hospital ya Bugando kwa ajili ya kuuaga.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo alisema kuwa wamechukua huo kwa kuwa mikusanyiko hairuhusiwi mkoani humo kutukana na hofu ya ugonjwa wa kipindupindu.

Aidha kamanda Mkumbo alieleza kuwa hawajawazuia kuuchukua mwili wa Mawazo na kwamba leo watawaruhusu kuuchukua lakini hawatawaruhusu kuuaga katika jiji hilo. 

“Sisi hatujawakataza kuchukua mwili, lakini tatizo hawa Chadema wanataka kuifanya kisiasa, “alisema Kamanda Mkumbo.

Viongozi wa kitaifa wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, aliyekuwa mgombea urais Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye wakifika jijini humo kushiriki kuuaga mwili wa Mawazo lakini walishindwa.

Mkuu wa idara ya Mawasiliano ya Chadema, Tumaini Makene alieleza kuwa chama hicho kimesikitishwa na katazo la Polisi na kueleza kuwa viongozi wa chama hicho walikuwa wanaendelea na kikao cha ndani kuhusu suala hilo. 

Ulinzi Mkali wa jeshi la polisi uliimarishwa katika hospitali ya Bugando ulikohifadhiwa mwili wa Mawazo kuhakikisha usalama na pia kuhakikisha viongozi wa Chadema hawauchukui mwili huo, zoezi ambalo lilifanikiwa. 

Zitto Kabwe Atoa 'Maksi' zake kwa Magufuli
Will Smith airudia Hip- Hop kwa nguvu kubwa, afunika 'Latin Grammy Awards'