Askari wa Jeshi la Polisi wawili wamefariki dunia huku wengine 9 wakijeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Iwambi, Kata ya Iwambi tarafa ya Iyunga jijini Mbeya,

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga ambapo amesema ajali hiyo  imesababishwa na mwendokasi wa dereva wa gari la polisi alipokuwa akitaka kuyapita magari mengine pamoja na utelezi.

“Chanzo cha ajali ni mwendokasi akijaribu kuyapita magari mengine pamoja na utelezi katika barabara. Upelelezi unaendelea. Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na majeruhi wamelazwa Hospitalini hapo. Taratibu za kusafirisha miili ya marehemu kwenda nyumbani kwao Iringa zinafanyika,”amesema Kamanda Mpinga

Hata hivyo, katika ajali hiyo, askari 09 walijeruhiwa ambapo kati yao majeruhi wawili wamelazwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na majeruhi saba wametibiwa na kuruhusiwa kurudi majumbani kwao Waliolazwa ni 1. H. 6952 PC KELVIN MARTIN Mkazi wa forest ameumia kichwani na 2. G. 3452 PC ADAM Mkazi wa Iganzo, Dereva.

Serikali yatoa tahadhari ugonjwa wa Chikuganya
Monalisa arudi kivingine, ashindanishwa tuzo bora Afrika