Polisi nchini Kenya imeanza kuwashughulikia wafuasi wa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga kwa kumkamata mbunge mmoja aliyehusika pakubwa katika hafla za kumuapisha kiongozi huyo wa upinzani.

Kukamatwa kwa mbunge huyo, Tom Kajwang wa upinzani kunajiri wakati ambapo serikali imefunga vituo vitatu vya runinga mbali na vile vya redio.

Aidha, Kukamatwa kwa kiongozi huyo kumejiri muda mfupi baada ya onyo kutoka kwa waziri wa usalama wa nchi hiyo kuwa watu wote waliohusika katika kumuapisha Raila Odinga watakamatwa na kushtakiwa.

Serikali imeshikilia msimamo wake kuwa kitendo cha Raila Odinga kujiapisha ni kitendo cha uhaini hivyo wote walihusika ni lazima washughulikiwe.

Hata hivyo, katika hatua nyingine Serikali nchini humo, imevifungia kurusha matangazo vituo vya runinga vya Nation Media Group NTV, Citizen TV cha kampuni ya Royal Media services Limited na KTN kwa kurusha matangazo ya mja kwa moja katika sherehe hizo mpaka pale uchunguzi utakapokamilika dhidi ya vituo hivyo.

 

 

Video: Lissu ahoji Polisi maswali 13 magumu, JPM atoboa siri ufisadi pasipoti
Auwawa na kuchunwa ngozi