Polisi wameanza uchunguzi kufuatia ajali ya moto iliyotokea katika soko la Gikomba nchini Kenya na kuharibu mali zinazokadiriwa kuwa na thamani ya mamilioni ya shilingi za Kenya.

Japo chanzo cha moto huo hakijabainika, Rais Uhuru Kenyatta ameagiza vymbo vya usalama kuanza uchunguzi mara moja nchini humo na kuharakisha uchunguzi huo kubaini kilichosababisha moto huo.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wafanyabiashara wa bidhaa katika eneo hilo wamesema kuwa moto huo ulianza kuteketeza vibanda vya samaki na nyama usiku wa kuamkia Ijumaa.

Hata hivyo, si mara ya kwanza soko hilo kuwaka moto, ambapo imekuwa kila mara moto unapozuka wafanyabiashara hupoteza bidhaa zenye thamani ya mamilioni, lakini kwa tukio hili wafanyabiashara wa soko hilo wameomba uchunguzi ufanyike mara moja.

Zitto Kabwe aing'ang'ania Serikali kuhusu mapato
Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 9, 2017