Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Justine Masejo amesema kikosi cha Mbwa na Farasi kimejipanga vyema kukabiliana na madawa ya kulevya na vilipuzi vya aina yeyote katika mkoa wa Arusha.

Kamanda Masejo ameseyama hayo hii leo agosti 12, 2022 wakati alipotembelea kikosi hicho kwa ajili ya kukagua mazoezi maalum ya mbwa ambao wanatumiwa na Jeshi la Polisi kuwatambua wahalifu mbalimbali wakiwemo wa madawa ya kulevya, silaha na mabomu.

Amesema, Jeshi hilo kupitia kikosi cha mbwa na farasi kinatoa mafunzo kwa mbwa wa kirai ilikuimarisha ulinzi na usalama katika mkoa wa Arusha huku Mkuu wa kikosi cha Mbwa na farasi mkoa wa Arusha ASP William Mwaisumo akisema kikosi hicho kimejipanga kutoa mafunzo kwa mbwa ili kuweza kuwatumia kumbua madawa na vilipuzi.

Basi la New Force lauwa mmoja sita majeruhi
Dkt. Mpango: Ajira za watoto Migodini zikomeshwe