Jeshi la polisi Kanda Maalumu  ya Dar es salaam kupitia kikosi cha kuzuia na kupambana na wizi  wa magari lime fanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili sugu kwa wizi wa magari, magari yaliyo kamatwa ni bus aina TATA no T.578 CGH na T.288 Toyota Carina.

Hayo yame semwa na Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam  Simon N.Sirro alipokua akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mapema hii leo,Sirro aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mulomba S/O Kabamba mkazi wa mbezi kimara na Alex S/O Alpha Lyimo mkazi wa kibaha pwani.

Sambamba na hao watuhumiwa wengine ni Dickson Mtalemwa(27)na Manase Yohana(27)wote wakazi wa pugu kwalala waliokamatwa kwa makosa ya kuvaa sare za jeshi la wananchi kinyume na sheria za nchi.

Aidha katika hatua nyingine kamishina Sirro  alitoa taarifa ya kikosi cha usalama barabarani kanda maalum ya Dar es salaam ya ukamataji wa makosa barabarani kuanzia tar 25/07/2016 hadi  tar 28/07/2016 kuwa jumla ya makosa yaliyo kamatwa ni 10,676 ambayo yali wezesha  kupatikana kwa kiasi cha fedha za tozo 320,280,000/=

Kiwanda Cha Dangote Chatozwa Faini Milioni 15
Video: Polisi Dar wakamata magari yaliyoibiwa