Njombe, kufuatia kusambaa kwa taarifa inayosemekana kuwa kundi kubwa la Askari polisi kuvamia nyumbani kwa mwandishi wa habari usiku wa manane na kumkamata mwandishi huyo Emmanuel Kibiki wa Gazeti la Raia Mwema.

Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, John Temu amekanusha madai hayo na kusema wao hawahusiki na kukamatwa kwa mwandishi huyo na kudai huenda akawa amekamatwa na taasisi nyingine ila si jeshi la polisi.

”Hakuna ukweli wowote ule kama kungekuwa na ukweli stori ingekuwa imeshafika kwetu ila inawezekana labda taasisi zingine za upelelezi zinafanya kazi zikawa zimemkamata maana taasisi za upepelezi huwa zinawakamata watu zenyewe, kwa hiyo watu wanapicha tu kuwa mtu akikamatwa basi jeshi la polisi ndilo linakuwa limemkamata.Kwa sababu kama sisi tungekuwa tumemkamata mpaka asubuhi hao polisi wangekuwa wamewasiliana na mkoa kutoa taarifa” amesema Temu

Aidha kwa mujibu wa taarifa za awali zinasemekana kuwa mwandishi huyo alivamiwa na askari ambao idadi yao haikujulikana na kulazimisha kuingia ndani kufanya upekuzi na kumkamata kwa kosa la kuandika habari za siasa.

”kosa lake ni kwamba anaandika sana mambo ya siasa na waliowatuma hawapendi. Wamemchukua tangu saa tisa usiku na hajarejea mpaka muda huu,” Tobina ambaye ni mke wa mwandishi huyo amenieleza kwa kilio cha kwikwi muda mchache uliopita” amesema Ezekiel Kamwaga amabaye ni mhariri wa Gazeti la Raia Mwema.

Emmanuel Kibiki amekuwa akifanya kazi mjini Makambako, Njombe na amekuwa akiandika mawazo yake katika mitandao ya kijamii na magazeti mbalimbali likiwamo Raia Mwema.

Utafiti wazitaja nchi zinazoongoza kwa rushwa sekta ya umma
Tanzia: Mtoto wa Cannavaro afariki dunia