Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu Dodoma, David Misime ametolea ufafanuzi wa taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kutoka ubalozi wa Marekani, ikionyesha kuwa na uwezekano wa kigaidi nchini na kwamba limeanza kufanyia kazi taarifa hiyo.

Katika taarifa iliyotolewa leo Januari 26, 2023 na David Misime imesema waraka huo ulisambaa jana January 25, 2023.

Amesema, pale itakapobainika uwepo wa jambo au watu wenye kutia shaka kutokana na mienendo yao  taarifa zitolewe haraka ili ziweze kufanyiwa kazi.

Aidha, Kamanda Misime amesema kuwa licha ya tahadhari hiyo lakini hali ya ulinzi na usalama hapa nchini  ni shwari na kwamba matukio makubwa yanayoweza kuleta hofu kwa wananchi yanaendelea kudhibitiwa.

CPB yamsimamisha kazi Mkurugenzi wake
Magaidi 11 wauawa, sita washikiliwa na Jeshi