Watu watano wamefariki na wengine 20 kujeruhiwa baada ya gari walilokua wakisafiria aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 938 DVQ lililokua likitokea Mkoani Mbeya kuelekea Mkoani Dar es Salaam kugongana na Lori la Mzigo lenye namba za usajili T. 693 DMF katika eneo la Iyovi wilaya ya Kilosa Barabara kuu ya Morogoro _Iringa .

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa Morogoro, Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva la Coaster ambaye jila lake halijafahamika kutaka kuyapita magari yaliyopo mbele yake bila kuchukua tahadhari.

Amesema, kwa sasa Jeshi la Polisi linamsaka dereva huyo ambaye mara baada ya kutokea ajali alikimbia kusiko julikana huku Kaimu Mganga Mfawidhi hospitali ya Mt. Kizito Mikumi, Dkt. Steven Mbilinyi akisema amepokea miili ya watu watano waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

Amesema, katika miili hiyo watatu wanaume na wanawake wawili huku majeruhi ishirini ambapo kati yao 10 wametibiwa na kuruhusiwa na 9 wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya St .Kizito na mmoja wamepelekwa hospitali ya Rufaa mkoa Morogoro kwa matibabu zaidi.

Maombi ya kazi 171,916 kada za Afya, Ualimu yapokelewa
Dullah Mbabe: Nitalipa kisasi kwa Katompa