Jeshi la Polisi la Mkoa wa Arusha limetoa huduma ya matibabu na ushauri wa kiafya katika kituo maalumu cha uleaji wa wazee wanaoishi katika mazingira magumu,AST, cha jijini Arusha.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha (TPF NET), Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mary Kipesha amesema msaada huo wa vitu mbalimbali umeendana na huduma za zafya katika mwendelezo wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Mwenyekiti wa mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha (TPF NET), Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP. Mary Kipesha akikabidhi msada huo.

Amesema, mbali na kutoa msaada huo, katika siku hizo 16 za kupinga ukatili amebainisha kuwa wametoa elimu katika shule, hospitali, nyumba za ibada, masoko pamoja na stendi za mabasi ambapo jamii imepata uelewa wa kutosha.

Awali, Mkurugenzi wa Kituo hicho, Bi. Ester Njau amelishukuru Jeshi hilo kwa kutoa matibabu kwa wazee wanaoishi katika kituo hicho ambapo amebainisha kuwa matibabu hayo pamoja na vitu mbalimbali vilivyotolewa vitaboresha afya za wazee hao.

Utoaji wa huduma ya Afya kwa wazee kama inavyoonekana katika picha ikiwa ne sehemu ya maadhimisho hayo.

Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Elerai Bwana Losioki laizer ameshukuru Jeshi la Polisi kwa kuwajali wazee wanaoishi katika mazingira magumu na kutoa wito kwa makundi mengine kuiga mfano ulioneshwa na Jeshi hilo.

Edna Lema arudisha ujumbe Young Africans
Rasmi Honour Janza aitema Namungo FC