Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar limelazimika kutolea ufafanuzi taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Jeshi hilo linamsaka aliyekuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad.

Taarifa hizo zilizosambwazwa zilieleza kuwa, Maalim Seif anatafutwa na jeshi hilo kwa kosa la kujitangazia ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu na kwamba hatua hiyo inachukuliwa kufuatia amri ya viongozi wa ngazi za juu visiwani humo.

Akingea na mtangazaji wa DW, Issac Gamba, Kamanda wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Kamishina Mkadam Khamis Mkadam amekanusha kupokea amri hiyo na kueleza kuwa taarifa hizo sio za kweli.

“Kwanza taarifa hizo nakanusha kwamba hazipo katika uhalisia wake. Lakini la pili pale [wananchi] wanapokuwa na mashaka yoyote.. mbona vituo vya polisi ni vya watu wote. Wafike waelimishwe kwa yale yote ambayo tunaweza kuyasema. Sijasikia Maalim Seif anahusishwa na tuhuma za aina yoyote, hivi ndivyo napenda niwaambie wenzangu,” alisema Kamishna Mkadam.

Msikilize hapa akieleza kwa kirefu:

Simba Yerejea Morogoro Kuweka Kambi
Unyama: Awachinja watu 14 wa familia yake wakiwemo wazazi na wanae