Jeshi la Polisi limesema litateketeza silaha haramu zilizosalimishwa kwa hiari katika kampeni maalumu iliyofanyika nchi nzima, kuanzia Septemba 1 – October 31, 2022 iliongozwa na kauli mbiu ya “Silaha haramu sasa basi, salimisha kwa hiari.”

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa Novemba 20 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi, SACP. David Misime imeeleza kuwa zoezi hilo lilitarajia kufanyika hii leo Novemba 22, 2022 katika Viwanja vya shabaha vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kunduchi, jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi, SACP. David Misime.

Aidha, taarifa hiyo imebainisha kuwa Mgeni rasmi katika zoezi hilo anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ambapo Wananchi na Viongozi wa Serikali za mitaa wamealikwa kujionea ufanisi wa zoezi hilo.

Serikali kutathmini upya utendaji wa TCRA-CCC
Argentina chali Kombe la Dunia 2022