Mabingwa watetezi wa Afrika Mashariki wa mchezo Pete (Netball) ya wanaume timu ya Polisi Zanzibar inatarajia kwenda Kampala Uganda kwenye mashindano hayo kutetea taji lao, mashindano ambayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake tarehe 26/03/2016.

Akizungumzia matayarisho yao kuelekea kwenye mashindano hayo katibu msaidizi wa timu hiyo Hamid Fadhil (Mnyamwezi) alisema wamejiandaa vizuri wao kama mabingwa watetezi katika mashindano hayo na hawana hofu yoyote juu ya mashindano, kwani vijana wake wapo vizuri ambapo siri kubwa kwao ya kufanya vizuri ni wachezaji wao wanacheza mpira wa Kikapu, hivyo inakuwa ni rahisi kwenye Netball.

“ Matayarisho yetu ni mazuri sana na naamini tutatetea ubingwa wetu huko Uganda ambapo najivunia sana wachezaji wangu wapo vizuri kwasababu wanacheza sana mpira wa kikapu na hii inakuwa rahisi kufanya vizuri kwenye Netball”. Alisema Hamid.

Kuanzia Mwaka 2003 Netball ya wanaume imeanza kushamiri Afrika Mashariki na kupelekea kuanzishwa mashindano hayo ambapo awali ilikuwa yanachezwa kwa wasichana pekee.

Zanzibar inafanya vizuri katika Netball ya wanaume ambapo katika mashindano hayo ya Afrika Mashariki inatoa upinzani mkubwa kutokana pia mchezo huo kwasasa unapendwa sana Visiwani na kupelekea kuongezeka timu nyingi zikiwemo mpaka za mitaani ikiwemo Sogea, Msabwen mbali na zile za Vikosi zikiwemo Polisi na JKU ambao pia wanafanya vizuri katika mchezo huo.

Chelsea Yatupwa Nje Barani Ulaya
Dk. Shein amtembelea Maalim Seif