Mshambuliaji kutoka nchini Zimbabwe na klabu ya Young Africans Donald Ngoma, ataondoka Jangwani mwishoni mwa msimu huu na kutimkia Afrika kusini.

Mtandao maarufu wa michezo wa nchini Afrika Kusini wa KickOff.com, umechapisha habari inayooeleza kuwa, mshambuliaji huyo yupo mbioni kumwaga wino wa kuichezea klabu ya Polokwane City ya nchini humo.

Chanzo cha karibu kabisa na klabu hiyo, kimesema Polokwane City inatarajia kukamilisha usajili huo hivi karibuni.

“Mazungumzo yamefikia katika hatua nzuri. Ngoma anaweza akamwaga wino muda wowote kuanzia sasa”. Kimesema chanzo hicho.

Ngoma alijiunga na Young Africans mwaka 2015 akitokea FC Platinums ya nyumbani kwao Zimbabwe na kutengeneza safu kali ya ushambuliaji na Mrundi, Amisi Tambwe ambayo imefanikiwa kuipa Young Africans mataji mawili ya ligi kuu Tanzania bara pamoja na kombe moja la michuano ya FA.

Kinda La Zambia Lajipanga Kuishangaza Dunia
Urusi yamdukua Rais wa Ukraine, Poroshenko.