Mfuko wa pensheni wa PPF umetoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni sita katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Mafinga Mkoani Iringa vitakavyosaidia kupunguza baadhi ya kero katika hospitali hiyo..
Msaada huo wa vifaa hivyo umekabidhiwa na Afisa Mawasiliano kutoka PPF, Lulu Mengele ambapo amesema kuwa msadaa huo ni muendelezo wa kurudisha huduma kwa wananchi kwa kile wanachochangia kwenye mfuko huo.
“Wananchi ambao wamekuwa wadau wetu wakubwa wamekuwa wakichangia katika mfuko wetu kitu kichosababisha turudishe fadhila kwa kuleta maendeleo ya moja kwa moja kwa wananchi hasa katika maeneo ambayo serikali imezidiwa na ukiangalia maeneo ya afya ndio imekuwa changamoto kubwa kwa serikali”.amesema Mengele
Aidha, amewataka wananchi kujiunga katika mfuko huo wa pensheni ambao umekuwa msaada mkubwa kwa wananchi hasa kwenye huduma ya afya kwa kuwa bima zao ni za bei nafuu.
 Hata hivyo, katibu wa Hospitali ya Mafinga, Bernard Makupa ameshukuru msaada huo wa vifaa tiba kutoka PPF kwa kuwa vifaa hivyo vitakuwa vimesaidia kupunguza kero mbalimbali katika Hospitali hiyo.

NASA wataka nafasi ya Msando apewe mtaalamu wa kigeni
Halmashauri Rukwa zaonywa dhidi ya matumizi mabovu ya mashine za EFD