Uchaguzi mkuu wa mwaka huu umekuwa na msisimko wa aina yake, msisimko ambao umegusa hata watu ambao sio raia wa Tanzania lakini wameamua kuwasapoti kwa nguvu wagombea wanaowapenda.

Rapa wa Kenya, Prezzo ameamua kumpa sapoti ya wazi mgombea urais wa CCM, Dkt. John Magufuli. Kupitia Instagram, rapa huyo ameeleza kupitia Instagram kuwa yeye anamsapoti Dkt. Magufuli kwa kuwa mama yake ni Mtanzania na anaipenda CCM.

“Nafatilia sana siasa za Tanzania kwasaabu mamangu ni Mtanzania na chama chake tangia zamani ilikuwa na bado ni CCM so sina budi Magufuli it is. Magufuli the rebirth of marehem Nyerere to the republic of Tanzania. #CCM #ChamaChaMapinduzi au ukipenda #ChamaChaMaendeleo #Rapcellency #TrulyUnruly,” aliandika kwenye post yenye picha ya Dk. Magufuli.

Napenda sana hizi rangi (KIJANI na NJANO) sijui Kwanini lakini nazipenda sana hizo rangi #Rapcellency #TrulyUnruly ?جاكسون مكيني?

A photo posted by Prezzo ?جاكسون مكيني? (@prezzo254) on

Prezzo ameendelea kupost picha kadha za kuisapoti CCM na mgombea urais wake.

Hii sio mara ya kwanza kwa Prezzo kujihusisha na siasa, mwaka 2013, rapa huyo alijitokeza na kumsapoti kwa nguvu Raila Odinga aliyekuwa anagombea urais wa Kenya.

Hivi sasa, Prezzo amehamia Tanzania akimsapoti Dkt. Magufuli ambaye ni rafiki wa dhati wa Raila Odinga.

Uchaguzi wa mwaka huu nchini umepata mashabiki hadi nchi za nje, bila shaka wapo wananchi wengi wa nchi jirani ambao ni mashabiki wa dhati wa wagombea urais wa Tanzania na watafurahi sana kuona upande wanaouunga mkono unaibuka kidedea.

 

Tim Krul Kuigharimu Newcastle Utd Hadi January 2016
Phil Jagielka Kuvaa Kitambaa Cha England