Mtoto wa mfalme wa Jordan, Prince Ali Bin Al Hussein ametangaza kuerejea tena kwenye kinyang’anyiro cha urais wa shirikisho la soka duniani FIFA ambacho kitafikia kilele mwezi Februari mwaka 2016.

Prince Ali ametangaza kurejea kwenye harakati hizo, kufuatia rais wa sasa Sepp Blatter kutangaza atajiuzulu nafasi yake mwanzoni mwa mwaka ujao, kutokana na kashfa ya mlungula iliyolikumba shirikisho la soka duniani FIFA tangu mwezi May mwaka huu.

Mdau huyo wa soka kutoka barani Asia, alitangaza nia ya kuingia tena kwenye mipango ya kuwania urais mbele ya waandishiwa habari mjini Petra, huku akionekana ni mwenye kujiamini.

Aliwahakikishai jamaa na rafiki zake ambao walihuhduria mkutano huo kwa kuwaambia bado anaamini ana nafasi nyingine ya kuwaaminisha wajumbe wa mkutano mkuu wa FIFA ili waweze kumchagua.

Alisema tayari wajumbe wa FIFA wameshafahamu yeye ni mtu wa aina gani na dhamira yake ya kutaka kuliongoza shirikisho la soka duniani imesimia katika ukweli na uadilifu, hivyo hana shaka katika harakati zake za kuwania kiti cha urais.

Prince Ali, mwenye umri wa miaka 39, alishindwa katika uchaguzi wa urais wa FIFA uliofanyika mwezi May mwaka huu, licha ya kumuonyesha upinzani wa dhati Sepp Blatter.

Prince Ali anakuwa mdau wa soka wanne kutangaza nia ya kuwania nafasi ya urais wa FIFA baada ya kutanguliwa na rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Michel Platini ambaye ni raia wa nchini Ufaransa, makamu wa rais wa shirikisho la soka barani Asia, Chung Mong-joon ambaye ni raia wa Korea kusini pamoja na gwiji wa soka duniani kutoka nchini Brazil, Arthur Antunes Coimbra Zico.

Magufuli Alia Na Posho, Ataja Mawaziri Wake Kwa Sifa
Roma Apata Hofu Baada Ya Kuchia Wimbo Wake Mpya ‘Viva’