Mshambuliaji kutoka nchini Zimbabwe, Prince Dube anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa majuma mawili, baada ya kuumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mwadui FC mwishoni mwa juma lililopita.

Mshambuliaji huyo ambaye alikosa michezo kadhaa kuanzia mwishoni mwa mwaka jana kabla ya kurejea mwezi uliopita, aliumia misuli ya paja dakika ya 25 kwenye mchezo huo, ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana mjini Mwadui.

Daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa amesema mshambuliaji huyo ambeya alisajiliwa Azam FC mwanzoni mwa msimu huu atakuwa nje kwa muda wa majuma mawili kabla ya kurejea tena uwanjani.

“Dube atakuwa nje kwa muda wa juma moja akipewa huduma na ile ya pili ataanza mazoezi mepesi ili kuweza kurejea kwenye ubora wake.”

“Baada ya kukamilisha majuma hayo mawili akiwa nje ya uwanja atafanyiwa vipimo tena ili kujua kwamba kama yupo fiti kurejea kwenye mechi za ushindani ama atapaswa kusubiri tena, ila mashabiki wasiwe na hofu kila kitu kitakuwa sawa.”

Mara ya kwanza Dube alivunjia mkono akiwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Young Africans uliomalizika kwa Azam FC kufungwa 1-0, Uwanja wa Azam Complex Chamazi, jijini Dar es salaam Novemba 2020.

Wasanii waipongeza konyagi kwa kutambua jitihada za wanawake
Mwambusi arithishwa mikoba Young Africans