Prince harry na mkewe Meghan wameanza ziara yao ya kwanza ya kiofisi nchini Australia, pia wanatarajiwa kutembelea miji ya Fiji, Tonga na New Zealand kwa muda wa siku 16.

Aidha, wanandoa hao wapya wa familia ya kifalme, hawajawahi kufanya ziara ya kiofisi tokea walipo oana mwezi wa tano mwaka huu,  ambapo wameamua kuanza ziara ya kwanza ya kikazi nchini Australia ikiwa ni kufuata nyayo za wazazi wa prince harry, prince charles na Diana ambao pia walianza ziara yao ya kwanza baada ya kufunga ndoa nchini Australia .

Walipo wasili nchini Australia walipokelewa na mwakilishi wa malikia wa Uingereza, Gavana General Peter Cosgrove katika bandari ya Sydney.

Kanye West akutana na Rais Museveni, ampa zawadi
Aliyemtwanga McGregor ataka kuzichapa na Mayweather

Comments

comments