Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema Kongamano la Kisayansi lililoshirikisha washiriki kutoka ndani na nje ya nchi linalenga kubadilishana uzoefu na nchi nyingine ikiwa ni pamoja na ubunifu katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali yaliyopo na yanaendelea kuibuka.

Waziri Ndalichako, amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Kongamano la tisa la Kisayansi la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS)

Amesema kuwa Serikali inategemea kupata maoni na mapendekezo ya namna ya kuendelea kuziwezesha taasisi za afya kufanya tafiti ambazo zitaendelea kuhakikisha kunakuwa na taifa lenye afya bora, kwani ni vigumu kufikia uchumi wa viwanda bila kuwa na watu wenye afya bora.

Aidha MUHAS imekuwa ikijiimarisha katika tafifi na sasa inajenga Kituo cha umahiri cha magonjwa ya moyo katika Kampasi ya Mloganzila ili kuendelea kufanya utafititi wa magonjwa moyo, sukari na shinikizo la damu.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la MUHAS Dkt. Harrison Mwakyembe amesema dunia ya leo imesongwa na magonjwa mbali mbali mapya na mengine sugu hivyo ni vizuri taasisi za utafiti kwa upande wa tiba, afya na sayansi Shirikishi zikafanya tafiti ili kuibua changamoto hizo.

“Tunauhitaji wa taasisi za utafiti upande wa tiba na afya na sayansi shirikishi ili mara kwa mara wafanye tafiti na kuibua hizo changamoto, ndio maana MUHAS ina Kongamano kama hili kila mwaka kuweza kubadilishana mawazo katika changamoto na tiba zinazopatikana duniani,” Amesema Dkt Mwakyembe

Hizi hapa sababu za makato ya miamala
Naibu Waziri Mahundi atoa maagizo kwa RUWASA