Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imewataka wananchi wote wanaoishi katika pori tengefu Loliondo wahame mara moja ili kupisha shughuli za uhifadhi na uboreshaji wa mazingira.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe katika hafla ya kuwatunuku vyeti wamiliki wa hotel zinazokidhi viwango vya ubora vya kuwalaza wageni jijini Arusha.

 Amesema kuwa, zipo hekari elfu mbili zilizotengwa na Serikali kwa ajili ya wananchi ambazo zimeshaelekezwa huduma muhimu lakini wananchi hao hawataki kukaa kule kwa sababu zao binafsi.
Aidha, amesema kuwa wananchi wamekuwa wakidanganywa na taasisi zisizo za kiserikali kuendelea kuishi katika maeneo ya pori tengefu la loliondo ambapo jambo hilo ni kinyume cha sheria ya uhifadhi.
Hata hivyo, ameongeza kuwa huduma muhimu za kijamii zimeshazogezwa katika eneo hilo ambapo hadi sasa wananchi wamekuwa wakisita kuhamia katika maeneo hayo na kuendeleza maisha yao jambo ambalo serikali inawataka kuhakikisha wanahamia katika maeneo ambayo serikali imewatengea.

Refa wa mpira wa miguu apigwa risasi na kupoteza maisha
IGP Sirro: Kustaafu kazi sio mwisho wa kufanyakazi jeshini