Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amefanya ziara ya ukaguzi katika ujenzi wa jengo jipya la Uwanja wa Julius Nyerere International Airport (JNIA) na kumhakikishia mkandarasi anayejenga jengo la uwanja huo ushirikiano wa bega kwa bega.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam  wakati wa ziara hiyo, ambapo amesema ameridhishwa na ujenzi wa jengo hilo hivyo amemhakikishia mkandarasi huyo kulipa madeni yote anayoidai Serikali kwa wakati muafaka.

“Nia yetu ujenzi huu ukamilike ifikapo Septemba mwakani, hivyo tunamtaka mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi na wasimamizi kumsimamia kikamilifu ili vifaa vinavyofungwa katika jengo hilo viwe na ubora uliokusudiwa na vidumu kwa muda mrefu,”amesema Prof. Mbarawa

Aidha, ameongeza kuwa kukamilika kwa jengo la uwanja huo kutawezesha kutoa huduma ya abiria zaidi ya milioni 8 na nusu kwa mwaka.

Hata hivyo, kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Prof. Ninatubu Lema amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa ujenzi huo utakamilika katika muda uliopangwa.

 

 

Video: Ni hatari Serikali kuanzisha Bodi ya Usajili wa Mawakili- Tundu Lissu
Jeshi la polisi lawaua wahalifu wanne Kibiti