Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa hii leo Mei 22, 2023 amevitaja vipaumbele 10 vya sekta ya Uchukuzi wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake Bungeni jijini Dodoma.

Vipaumbele hivyo ni pamoja na i. Mradi wa Uboreshaji wa Usalama wa Usafiri katika Ziwa Victoria – Shilingi bilioni 1.73.

ii. Mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam – Shilingi bilioni 93.80.

iii. Mradi wa Ukarabati wa Njia Kuu ya Reli Iliyopo (MGR) – Mradi wa Tanzania Intermodal Railway II – Shilingi bilioni 11.72.

iv. Mradi wa Ujenzi wa Reli Mpya ya Standard Gauge – Shilingi trilioni 1.113.

v. Mradi wa Ununuzi wa Rada, Vifaa na Ujenzi wa Miundombinu ya Hali ya Hewa – Shilingi bilioni 13.00.

vi. Mradi wa Uboreshaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) – Shilingi bilioni 300.00.

vii. Mradi wa Ujenzi wa Meli Mpya na Ukarabati wa Meli – Shilingi bilioni 100.00.

viii. Mradi wa Kuboresha Miundombinu na Ununuzi wa Vifaa vya Kufundishia – Shilingi bilioni 2.27.

ix. Mradi wa Uboreshaji wa Reli ya TAZARA- Shilingi bilioni 13.19 na

x. Mradi wa Ununuzi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege na Uendelezaji wa Chuo cha Mafunzo ya Usafiri wa Anga – Shilingi bilioni 6.5.

Mashabiki Ruvu Shooting waombwa radhi
Pep Guardiola arudisha shukurani kwa Mashabiki