Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa amezindua mradi mkubwa wa uboreshaji wa huduma ya maji mjini Mbinga akiwa katika ziara yake kikazi mkoani Ruvuma.

Katika uzinduzi huo, amesema kuwa mradi huo ni hatua ya Serikali kufikia lengo la kufikia asilimia 90 kwa miji mikuu ya wilaya itakapofika mwaka 2020, na imepanga kutumia shilingi Bilioni 1.2 kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji kwa miji mingine 25 Tanzania Bara na Visiwani.

Amesema kuwa mradi huo utabadilisha kwa kiasi kikubwa maisha ya wananchi wa Mbinga sio tu kwa kutoa huduma ya majisafi na majitaka kwa wananchi.  pia ni muhimu kwa shughuli za kila siku za kiuchumi zinazofanyika katika mji huo.

Aidha, Prof. Mbarawa ameipongeza Mamlaka ya Maji ya Songea Mjini (SOUWASA) kwa kazi nzuri ya kusimamia mradi huo mpaka umekamilika.

Mradi huo upo chini ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya mji wa Mbinga (MBIUWASA) ulianza kujengwa Mei, 2017 chini ya mkandarasi Almasi General Supplies Ltd ya Songea na kuanza kutoa huduma ya maji kwa mji wa Mbinga Februari, 2018 umegharimu   Shilingi Bilioni 1.029.

Kwa upande wake Meneja wa MBIUWASA, Patrick Ndunguru amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kumeleta ongezeko la uzalishaji wa maji kutoa wastani wa lita 700,000 wakati wa kiangazi na lita 1,600,000 wakati wa masika, ikichangia kuongeza mapato kutoka Shilingi Milioni 18 hadi Milioni 25 kwa mamlaka hiyo.

 

Video: Mo Dewji aibua shida mpya, Waziri apinga ripoti ya polisi
Flyover nyingine kubwa, yaanza kujengwa Dar