Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema uamuzi wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), wa kutokutangaza Shule bora kupitia matokeo ya mwisho ya mitihani yanatokana na utata wa namna ya kutathmini.

Mkenda ametoa kauli hiyo hii leo Februari 01, 2023 Bungeni jijini Dodoma, kufuatiwa kuombwa kwa mwongozo na Mbunge wa Jimbo la Bunda, Mwita Getere ambapo ametumia mifano mbalimbali kulielezea suala hilo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda.

Amesema, “mfano wa Shule yenye Wanafunzi 100 na nyingine ina Wanafunzi 20 waliomaliza kidato na nne, ya Wanafunzi 100, 70 wamepata A, 30 hawakupata A na yenye Wanafunzi 20 wote wamepata A, kwa kuangalia wastani wa ufaulu yenye Wanafunzi 20 itatangazwa kuwa Shule bora lakini wengine wanaweza kuona yenye Wanafunzi 70 wenye A ndio iwe Shule bora.”

Aidha, amesema aina hiyo ya tathmini inaweza kupelekea shinikizo kwa Shule yenye Wanafunzi mathalani 100 kwa kuondoa wale 30 ambao hawakupata A, ili iweze kutangazwa Shule bora kwa kupata A zote ambazo ni asilimia 100 na kwamba hata hivyo takwimu zote zipo hadharani.

Tanzania na Finland zajadili maslahi ya kiuchumi
Ruvu Shooting yakimbilia Jamhuri Morogoro