Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wametakiwa kujitathmini kutokana na kadhia ya kushindwa kusimamia mradi wa maji Wilayani Rombo.

Mbunge wa Jimbo la Rombo ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prf Adolf Mkenda ametoa kauli hiyo akiwa katika muendelezo wa ziara jimboni humo ambapo amesema RUWASA wanamhujumu waziri wa maji Jumaa Aweso.

“Tatizo namba moja, mbili, na tatu Rombo ni maji sasa mtu anayechezea mradi wa maji sielewi ana madhumuni gani na anataka wananchi wa Rombo wawe na taswira gani kwa serikali, wanamhujumu Waziri wa Maji Mhe Juma Aweso ambaye ni mchapakazi na kwa hili nitamualika aje aone changamoto hii” amekaririwa Prof Mkenda.

Mradi huo ambao Ulisainiwa na mkandarasi ili kuanza kazi mwanzoni mwa mwaka 2022, lakini mpaka sasa hakuna kazi iliyofanyika zaidi ya kuwekwa mchanga na kokoto zisizozidi gari moja.

Prof Mkenda amesema mradi huo utakapokamilika utarahisisha upatikanaji maji kwa lita Milioni 4 kwa siku na kupunguza tatizo la maji linaloikabili Wilaya ya Rombo.

Amesema kuwa Mradi huo ni sehemu ya miradi ya maji yenye jumla ya Bilioni 10 iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Wilayani Rombo.

“Kwa kuwa sehemu hiyo ni ngumu kufikika sio rahisi kwa viongozi kufika na kuona maendeleo ya mradi huo inakuwa rahisi kuficha mapungufu haya kwa hiyo RUWASA inabidi ijiangalie upya kwa kuwa ndio msimamizi wa mradi huo,” amesisitiza Prof Mkenda.

Prof. Adolf Mkenda ambaye ni mbunge wa Jimbo la Rombo Mkoani Kilimanjaro amemuomba Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi Clement Kivegalo kutembelea Rombo ili kujionea kadhia za ucheleweshaji wa miradi ya maji kwa kuwa RUWASA inatia shaka katika usimamizi wake wa miradi hiyo.

Florent Ibenge aihofia Young Africans kimataifa
Wananchi wasogezewa huduma za meno